Wednesday, July 30, 2014

AJALI YA BASI YAUA 20 DODOMA


Basi la Moro Best baada ya ajali hiyo mbaya.

Picha 4 za Kimahaba za Wema Sepetu na Ommy DimpozWema  Akiwa  na  SHEMEJI  yake  ndani  ya  pozi  matata

GARI LA DUDE LAKAMATWA KWA UJAMBAZI

GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.

ABOUBAKAR SADIK APASULIWA

AFYA ya mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar Sadik ambaye anatumikia Radio One Sterio ya jijini Dar es Salaam, si nzuri kiasi cha kulazimika kufanyiwa upasuaji haraka.

Tuesday, July 29, 2014

Sangoma Amfyeka Nyeti Mtoto wa Mwaka Mmoja na Kutoweka Nayo


Ni jambo lililowaacha midomo wazi madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambapo mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (pichani akiwa na muuguzi) kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa nyeti na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji ‘sangoma’ na kuipeleka kusikojulikana.

Askofu: Waziri Chikawe hana ubavu wa kulifunga Kanisa la Moravian
Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian nchini, Alinikisa Cheyo amesema Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe hana ubavu wa kulifuta kanisa lake.

UPDATE: Taarifa ya kusitishwa kwa Ajira za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji iliyotolewa jana na Wizara ya mambo ya ndani haihusiani na Ajira 70 za Mkaguzi msaidizi wa UhamiajiBaadhi ya Vyombo vya Habari leo tarehe 29 Julai, 2014 vimeandika kwa makosa kuwa ajira za Uhamiaji zilizositishwa jana zinahusiana na 70 zilizopatikana baada ya usaili uliofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Swala ya Eid El Fitr Yaswaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.

Monday, July 28, 2014

Picha Tatu za Bahati Bukuku akiwa Hospitalini baada ya kupata Ajali mbaya ya GariNyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi.

Hongera Ray C: Video Queen wa wimbo wa Ice Cream aanza kupona UTEJA Uliosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya
Mrembo  Doreen  aliyekuwa  video  Queen  wa  wimbo  uliotokea  kutamba  miaka  ya  nyuma  wa  Ice  Cream  ulioimbwa  na  Haji  Nura  'Noorah'  akimshirikisha  Suma  Lee  ameanza  kurejea  katika  hali  yake  ya  kaaida  ikiwa  ni  baada  ya  kutopea  katika  matumizi  ya  dawa  za  kulevya.....

Wanafunzi Watano WALAWITIWA Kwa Mpigo na MwenzaoJeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la sita kwa tuhuma nzito ya kuwalawiti wenzake watano kwa mpigo.

Makanisa Yanayoendekeza Vurugu Kufutiwa USAJILI Wake


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amesema yeye mwenyewe atayafuta makanisa yote yanayoleta vurugu na uvunjifu wa amani kwa kuwa hayatoi taswira ya kile wanachopaswa kufanya na ni aibu kwa Mungu  wanayemtumikia.
 
Amesema ni aibu kwa viongozi wa makanisa kupigana hadharani wakati wa Ibada na kupishana katika vituo vya Polisi wakishtakiana jambo alilosema linachochea shari na kuharibu nchi.
 
Amelitaja kanisa mojawapo ambalo lina vurugu kuwa ni Kanisa la Moravian, Jimbo la Misheni Mashariki ambalo kwa zaidi ya miaka miwili sasa sharika zake zimekuwa na vurugu inayohusisha uongozi na ubadhirifu wa mali.
 
"Serikali haitavumilia vitendo vya vurugu katika makanisa na ikibidi mimi mwenyewe nitafuta usajili wa hayo makanisa yenye migogoro kuepusha shari," alisema Chikawe jana katika ibada maalumu ya kuombea Taifa amani, utulivu na uzalendo wa kweli.
 
Hivi karibuni kanisa hilo wilayani Kinondoni, waumini walipigana na sasa kuna kesi kuhusu ugomvi huo katika vyombo vya Sheria.
 
Maombi hayo yaliandaliwa na Chama cha Kitume cha Karismatiki Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Kituo cha Maombi na Maombezi cha Emaus, kilichopo Ubungo, jijini humo.
 
Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi akiwakilisha viongozi wa Serikali na kisiasa katika maombi hayo yaliohusisha pia kuombea mchakato wa Katiba, vita dhidi ya rushwa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani, alisema viongozi wa dini wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuchochea amani ya Taifa, lakini inashangaza baadhi yao wanaongoza kwa kuleta vurugu.
 
"Kwa bahati mbaya migogoro katika makanisa na madhehebu mbalimbali imekuwa mingi wakati huu na sababu za migogoro hiyo ni pamoja na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na ubadhirifu wa mali za kanisa, mathalani Kanisa la Moravian Tanzania, lipo katika mgogoro mkubwa hivi sasa kiasi cha watu kupigana hadharani.
 
"Wanapigana wakati wa ibada, tujiulize ni mfano gani tunawaonesha Watanzania wasio na dini, kwa utaratibu huo nani atatamani kuwa Mkristo, natumia fursa hii kuwakumbusha viongozi kuwa mfano wa kuigwa, viongozi ni  lazima  tuwe na hofu ya Mungu na tutumie nafasi zetu kujenga umoja, amani na mshikamano," alisema Chikawe.

WACHENI KUWAHARIBU WANAFUNZI WA KIKE!!!!! ONA HII ADHABU ALIYOPEWA HUYU JAMAA


Jamaa mmoja huko Ghana (mfanyakazi wa Benki fulani) amenaswa akiwalamba wanafunzi wa kike ndai ya gari lake katika shule moja ya kimisionary nchini humo. Hiyo hapo juu ndo moja ya adhabu alizopewa

MASIKINI HUSSEIN MACHOZI!!!!! AKIPATA CHA MOTO BAADA YA KUCHEPUKA NA MKE WA KIGOGO MWANASIASA WA KENYA

Machozi Hussein
Chonde chonde wasanii wetu, mtakuja kufa/kuwawa kama hamtabaki katika njia kuu zetu, ona kilichompata

HII SMS YA DJ MANYWELE INAWEZA KUKUONGEZEA SIKU ZA KUISHI KWA KUVUNJIKA MBAVU!!! ISOME